BREAKTHROUGH KISWAHILI DARASA LA 7

KSh 550

Primary Breakthrough Workbook Kiswahili 7

Msururu wa vitabu vya Breakthrough Workbooks ni wa kipekee! Vitabu hivi vya mazoezi vimeundwa kukidhi matakwa ya wanafunzi na walimu na pia kuwapa wazazi fursa nadra ya kushughulika na masomo ya watoto wao kwa kuwapa kazi za ziada nyumbani.Faida za vitabu hivi vya mazoezi hazihesabiki na ni pamoja na:

Faida kwa Mwanafunzi:

  • Vimesheheni mazoezi kemkem na karatasi za marudio ili kuwaandaa wanafunzi kwa mitihani yoyote
  •  Wanafunzi wanaweza kufanya mazoezi peke yao bila usaidizi wa mtu yeyote kwa hivyo wanaweza kujitathmini uelewa wao vyema
  •  Picha na michoro mwanana itafanya mwanafunzi aelewe vyema yanayofunzwa.

Out of stock

Compare

Description

Faida kwa Mwalimu:

  •  Vinampatia mwalimu kazi ya ubaoni tayari na kwa hivyo kumsaidia kuokoa muda angetumia kuandika mazoezi ubaoni
  •  Ni rahisi kutathmini wanafunzi kila siku kwa kurejelea kurasa za kitabu hiki kwani mazoezi yanaambatana na mpangilio wa silabasi
  •  Vitabu vya majibu viko kando kwa hivyo wanafunzi hawawezi kunukuu majibu ya mazoezi
  •  Mazoezi yanakidhi haja za wanafunzi wanaoelewa mambo kwa haraka na pia wale wanaoelewa mambo polepole

Faida kwa Mzazi:

  • Vinawapa wazazi mazoezi mengi yanayowasaidia kutathmini maendeleo ya watoto wao masomoni
  •  Si lazima mzazi awe mtaalamu wa somo lolote ili kumsaidia mtoto wake kimasomo kwa sababu majibu ya maswali yote ya mazoezi yako katika kitabu cha majibu (kando na cha mazoezi)
  • Vinatia nguvu uhusiano kati ya wazazi na walimu, wote wanapojitahidi kuboresha masomo ya wanafunzi
X